Breaking News

China yaimarisha Ushirikiano baina yake na Afrika

Mugabe and Xi-Jinping

Kongamano la pili la uwekezaji barani Afrika limemalizika jana jijini Guangzhou, China ambapo kampuni za China na Afrika zimesaini makubaliano ya uwekezaji yenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 25.

Katika miaka ya hivi karibuni ushirikiano kati ya China na Afrika umeelekea kwenye uwekezaji na viwanda vya kuongeza thamani ya bidhaa kutoka biashara ya moja kwa moja. Aidha, kampuni za China zinashiriki zaidi kwenye kuendesha miundombinu na maeneo maalum ya viwanda barani Afrika na huduma za fedha, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo zilifanya kazi za ukandarasi wa miradi ya ujenzi.

Miradi iliyosainiwa kwenye mkutano huo ni pamoja na uzalishaji wa umeme kwa kutumia muhogo na mua, na uendeshaji wa bandari ya Mombasa.