Kumekuwa na mjadala kama huo katika jeshi la Marekani
Mwanamke mmoja amekuwa mtu wa kwanza katika
Umoja wa Falme za kiarabu kuwasilisha ombi la kutaka kubadilishwa
jinsia chini ya sheria mpya inayohalalisha upasuaji wa kufanyia
mabadiliko sehemu za siri .
Wakili
wa mwanamke huyo Ali al-Mansouri ameambia vyombo vya habari nchini humo
kwamba siku zote mteja wake amehisi kuwa yeye ni mwanamume, na amekuwa
akipokea matibabu ya kimwili na kiakili kwa miaka minne iliyopita.
Ameeleza
kuwa hisia za mteja wake ni kwamba mwili wake haudhihirishi jinsia yake
ya kweli na ni jambo lililomsababishia wasiwasi na mawazo mengi.
Mansouri ameeleza kuwa tume ya matibabu ilipendekeza kwamba afanyiwe upasuaji huo.
Sheria
hiyo mpya ya afya ya Umoja wa falme za kiarabu ilioidhinishwa mapema
mwezi Septemba, inaruhusu upasuaji huo kwa misingi ya matibabu.
"upasuaji
huo... Unaruhusiwa iwapo ni sehemu ya matibabu kwa matatizo ya kijinsia
, kama itakavyoshauriwa na tume ya matibabu itakayoundwa kwa lengo
hilo," sheria hiyo inasema.
Mahakama ya Abu Dhabi itasikiliza kesi hiyo tarehe 28 mwezi Septemba.
Awasilisha ombi la kubadili jinsia yake Arabuni
Reviewed by Mipiko
on
3:33 AM
Rating: 5