Afya ya Hillary Clinton yatengamaa.
Mgombea
Urais kupitia Chama cha Democratic nchini Marekani Bi Hillary Clinton
amerejea kwenye mbio za kampeni baada ya kuugua homa ya mapafu.
Akiongea
na mwandishi wa habari akiwa kwenye ndege kuelekea Greensboro North
Carolina, Bi Clinton alisema anajiskia vizuri baada ya mapumziko ya siku
tatu.
Mpinzani wake wa Chama cha Republican, Donald Trump ametoa barua kutoka kwa daktari wake ikionesha kuwa ana afya njema.
Barua
hiyo inaonesha kuwa anatumia dawa ili kupunguza unene na kiwango
kilichopitiliza cha uzito, lakini hatumii kilevi wala kuvuta sigara.


