TANZIA: Mchezaji wa Simba SC aliyewanyanyasa West Bromwich Albion afariki dunia
Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Sunderland (Simba SC) na Taifa Stars, Arthur Mambeta amefariki dunia jioni ya jana siku ya Jumatano kufuatia kuugua kwa muda mrefu.
Mambeta alikuwemo kwenye kikosi cha First Eleven ya Afrika Mashariki iliyocheza na timu ya West Bromwich Albion ya Uingereza mwaka 1968 kisha akakipiga dhidi ya wageni hao akiwa ndani ya kikosi cha Dar Combine. Nyota huyo aliyekuwa hatari wakati wa zama zake aliikabili tena West Bromwich Albion akiwa ndani ya kikosi cha Tanzania XI na alipata nafasi ya kucheza safu ya ushambuliaji kwa takribani miaka nane kabla haja tangaza kustaafu soka mwaka 1973. Tukio kubwa kwa wadau wa mchezo wa soka ambalo hawawezi kulisaha ni pale aliporeiea tena katika soka na kuchezea nafasi ya beki wa kutumainiwa badala ya ile ya hawali iliyo zoeleka hii ikifuatiwa na klabu ya Simba kumshawishi kurejea baada ya beki wao Juma Mzee kugoma wakati wa kijiandaa dhidi ya hasimu wao Yanga SC mchezo wa ligi kuu. Ambapo katika mchezo huo aliweza kumkaba vema na kumnyamazisha mchezaji hatari wa wakati huo wa Yanga SC, Kitwana Manara na kufanikiwa Simba SC kuchomoza na ushindi wa bao 1- 0 lililofungwa na Haidary Muchacho baada ya hapo nafasi yake ikarithiwa na Omar Gumbo Mwenyezimungu amrehemu.