Breaking News

PIQUE AWAJIBU WANAOMPAKAZIA KUHUSU KUACHANA NA SHAKIRA


Gerrard Pique amewajibu wabaya wake wanaompakazia kuhusu kutengana na mkewe Shakira baada ya kuibukia katika mazoezi ya mwanamuziki huyo nyota duniani.

Kwa takribani wiki kadhaa kumekuwa na taarifa za beki huyo wa kimataifa wa Barcelona na Hispania kutengana na mkewe waliyezaa watoto wawili.

Lakini kwa mara ya kwanza, mchezaji huyo amevunja ukimya kwa kuweka picha ikimuonyesha akiwa kwenye mazoezi ya Shakira.

Mashabiki wa soka Hispania wamekuwa wakimdhihaki Pique uwanjani kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na Shakira, lakini hakuwahi kuwajibu.

Picha hiyo inamuonyesha Pique akiwa ameweka kidole mdomoni ikiwa ni ishara ya kuwataka wabaya wake kukaa kimya huku Shakira akiendelea na mazoezi.

Pique na Shakira walianzisha uhusiano mwaka 2010 nchini Afrika Kusini wakati mwanamuziki huyo alipokwenda kutengeneza wimbo wa Kombe la Dunia.

Mchezaji huyo alianza kuonja shubiri, baada ya kupaza sauti akitaka kujitenga kwa Jimbo la Catalunya, kauli ambayo imeibua hisia kubwa kwa mashabiki wa soka nchini humo.