Breaking News

MASENETA WA MAREKANI WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUKUTANA NAO....WAFUNGUKIA FURSA MUHIMU ZA KUKUZA UCHUMI ZILIZOPO TANZANIA


Maseneta wa Baraza la Seneti la Marekani wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Rais John Magufuli Iluku jijini Dar es Salaam leo. Picha na Ikulu 

Rais John Magufuli wa Tanzania, amefanya mazungumzo na ujumbe wa maseneta wa Baraza la Seneti la Marekani.


Taarifa ya Ikulu ya leo Jumatano imesema maseneta hao ni wajumbe wa kamati ya mazingira inayoshughulikia hifadhi ya taifa, wanyamapori na misitu ya Marekani.


Maseneta hao wamekuwepo nchini Tanzania kwa siku tatu lengo likiwa ni kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.


Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk Inmi Patterson.


Taarifa ya Ikulu imewataja maseneta hao kuwa ni James Inhofe, Mike Enzi, David Perdue, Luther Strange, Tim Scott na John Thune.


Baada ya mazungumzo, kwa nyakati tofauti maseneta James Inhofe na Mike Enzi wamemshukuru Rais Magufuli kwa kukutana nao.


Pia, wamemshukuru kwa kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Marekani kuja kuwekeza nchini.


Maseneta hao wamesema Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo ni fursa muhimu ya kukuza uchumi.