PICHA:RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WAWILI AKIWEMO NAIBU MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Oktoba 2017, amemuapisha Meja Jen. Issa Suleinam Nassor kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.
Mara baada ya kula kiapo, Balozi Issa Suleinam Nassor amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha imani kwake na kumteua kushika nafasi hiyo na amemuahidi kuendeleza na kukuza uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Misri.
Kwa upande wake Balozi Abdulrahman Kaniki amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kumteua kushika nafasi hiyo na ameahidi kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Zimbia ulioasisiswa na Hayati Baba wa Taifa Mw. Julius Kambarage Nyerere na Dkt.Keneth Kaunda.