MBUNGE JOSEPH MSUKUMA AKAMATWA NA POLISI GEITA
Polisi mkoani Geita wanamshikilia Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku (Musukuma) kutokana na vurugu zilizotokea eneo la mgodi wa GGM Septemba 14 mwaka huu.
Mbunge Msukuma na madiwani wa wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia kwenye mgodi wa GGM wakishinikiza kulipwa dola 12 milioni zinazotokana na kodi ya huduma.
Kamanda wa polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kukamatwa kwa Msukuma na kusema askari walimkamata katika eneo la CCM mjini Geita.
Kamanda amesema kukamatwa kwa Msukuma ni mwendelezo wa Polisi kuwakamata watu wote waliohusika katika vurugu zilizotokea Septemba 14.
Amesema tayari wamekamata madiwani wengine wawili na wananchi watano na kwamba jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi na msako wa kuwakamata wote walioshiriki.
“Bado tunaendelea na msako na hawa ni wahalifu kama wahalifu wengine na sheria lazima ichukue mkondo wake na Msukuma tumemkamata sio kwamba amekuja mwenyewe ”amesema
Kamanda amesema kwa sasa wanaendelea na mahojiano na wakikamilisha sheria itachukua mkondo wake na kwamba kosa la jina halina kikomo na wote walioshiriki vurugu za kufunga barabara lazima wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria .
Hadi sasa jeshi la polisi mkoani Geita linawashikilia madiwani kumi wa halmashauri za wilaya ya Geita waliofunga barabara zinazoingia mgodi wa GGM na kuharibu miundo mbinu ya maji yaliyotengenezwa na GGM kwa ajili ya shughuli za mgodi na wananchi wa mji wa Geita katika kijiji cha Nungwe jambo ambalo ni kinyume na sheria.