Breaking News

LEMA AMJIBU WAZIRI WA AFYA,BAADA YA SERIKALI KUKUBALI KUGHARAMIA MATIBABU YA LISSU


Mbunge wa Arusha Mjini Gobless Lema amemjibu Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu kauli aliyotoa jana kuwa serikali ipo tayari kumtibu Lissu endapo familia yake itaomba kwa serikali, Lema amesema kuwa familia ya Lissu haijashindwa kumgharamia matibabu.

Lema amesema kuwa anaamini familia ya Tundu Lissu ni Watanzania wote ambao wanapenda haki na Demokrasia ndani ya nchi, na wote ambao wanaumizwa na jambo hilo bila kujali itikadi zao hivyo watachanga shilingi moja moja kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu na hata ikibidi mali zao watauza ili kuweza kumuwezesha Tundu Lissu kupata matibabu.


"Familia ya Lissu ni Watanzania wote wanaopenda utawala wa sheria, Utawala wa Demokrasia, familia ya Lissu ni Watanzania wote bila kujali itikadi zao ambao wanajisikia vibaya kwa matendo ya kihalifu kwa wabunge kupigwa risasi hadharani na bunge lisichukue hatua stahiki hii ndiyo familia ya Lissu, mtu yoyote ambaye anaguswa na ubinadamu na familia hii haijashindwa kumlipia matibabu tutachanga shilingi moja moja ikiwa ni lazima sana tutauza hata mali zetu kuhakikisha kwamba Mhe. Tundu Lissu akosi fedha za matibabu" alisema Godbless Lema.