KENYA:TAREHE YA UCHAGUZI WA MARUDIO YASOGEZWA MBELE
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), imebadilisha tarehe ya kufanyika uchaguzi wa marudio na kwamba badala ya Octoba 17 sasa utafanyika Oktoba 26.
Awali, Mahakama ya Juu nchini Kenya chini ya Jaji Mkuu David Maraga kufuta matokeo ya uchaguzi wa awali uliompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Oktoba 17, siku 60 baada ya uamuzi wa
Kupitia taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya IEBC , Wafula Chebukati imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa ili kuipa IEBC muda wa kujiandaa zaidi na hasa katika masuala ya teknolojia.
“Ni dhahiri kuwa, kufutwa kwa uchaguzi kumeleta athari na hasa kwenye teknolojia itakayotumika. Ili kuhakikisha tume inajiandaa kuleta uchaguzi wenye viwango vinavyohitajika na Mahakama ya Juu, tunapenda kuujulisha umma na wadau wote kuwa uchaguzi mpya utafanyika Alhamisi Oktoba 26.”
Tume pia imesema itayapitia maagizo ya Mahakama ya Juu kuhusu uchaguzi wa marudio.
Mahakama ya Juu nchni humo ilifuta matokeo ya Urais yaliyompa ushindi Rais Kenyatta kuwa madarakani kwa muhula wa pili, matokeo hayo yalifutwa Septemba 1 mwaka huu.