Breaking News

  

WAKENYA WAASWA KUWA NA UTULIVU WA KISIASA KUFUATIA VUGUVUGU LINALOENDELEA NCHINI HUMO



Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ametoa wito kwa viongozi wa Kenya kuwajibika kwa kutuliza mvutano wa kisiasa.

Kamishna huyo amesema Kenya iko kwenye wakati mgumu, hivyo viongozi wa kisiasa wa nchi hiyo wanatakiwa kujitahidi wanavyoweza kutuliza mvutano wa kisasa. Ameongeza kuwa, kama kuna madai kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi, yanapaswa yawasilishwe kwa njia za kikatiba na kisheria.

Aidha, Al Hussein ameeleza wasiwasi wake kuhusu ripoti kuwa vikosi vya usalama nchini Kenya vimetumia silaha za moto dhidi ya waandamanaji, na kuhusu ripoti za matumizi ya nguvu yanayofanywa na polisi yaliyosababisha vifo na majeruhi ya watu kadhaa.