NEYMAR AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE MAPYA AKIWA PSG
Akiweka mbali kabisa na kusahau maisha Camp Nou, tayari Mbrazili huyo ameanza kujiona yuko nyumbani ndani ya Paris.
Neymar alithibitisha kuwa ametulia katika klabu yake mpya ya PSG. Alikiri kuwa ilikuwa vigumu kwake kuondoka Barcelona, lakini kwa sasa anasema amefurahi kuwa Ufaransa.
Alisema anafahamu kwamba wengi walifikiri kuondoka kwake Barcelona ndiyo mwisho wake, lakini mambo kulingana naye yamekuwa ni tofauti kwani katika PSG yeye anajiona kama mchezaji aliyezaliwa upya.
Mshambuliaji huyo wa timu ya soka ya taifa ya Brazil anasisitiza kuwa anafurahi na kuendelea kucheza soka kwa kiwango kile kile, huku akibainisha kuwa kilichobadilika ni nchi, mji na timu tu.