Breaking News

RAIS MAGUFULI ARIDHIA MAOMBI YA KUSTAAFU KWA JAJI RUHANGISA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Prof  John Eudes Ruhangisa.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Prof. John Eudes Ruhangisa kuanzia tarehe 06 Julai, 2017.

Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga.