MASHABIKI 8 WAFARIKI KATIKA UWANJA WA SOKA SENEGAL
Watu wanane wamefariki dunia baada ya kukanyagana walipokuwa wakishuhudia michuano ya ligi ya soka nchini Senegal.
Waziri wa Michezo wa Senegal, Matar Ba, amesema msichana mdogo ni miongoni mwa waliopoteza maisha na majeruhi 60 wamefikishwa hospitali mjini Dakar.
Habari zinasema mashabiki wa timu mbili za mpira wa miguu zilizokuwa zinacheza walianzisha vurugu hiyo kwa kushambuliana baada ya mchuano uliochezewa katika uwanja wa michezo wa Demba Diop Stadium kumalizika.
Katika vurumai hiyo, sehemu ya ukuta wauwanja huo iliporomoka wakati idadi kubwa ya watu walipokuwa wakisukuma kuondoka uwanjani hapo. Serikali imeahidi kuchukua hatua madhubuti ili kuzuia matukio kama hayo kutokea tena nchini Senegal.