Breaking News

VIDEO:RAIS MAGUFULI AWATOA HOFU POLISI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutumia weledi ili kuleta kuendelea kulinda amani na kukomesha mauaji dhidi ya raia huku akiwatoa hofu askari wa jeshi la polisi kuwa kero zao zinazowasumbua tayari zipo kwenye mikakati ya kutatuliwa.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Magufuli amesema hayo jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na makamanda wakuu kutoka makao makuu ya polisi, Makamanda wa Mikoa na vikosi vya Tanzania bara na Zanzibar na viongozi wote wakuu wa polisi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Hata hivyo Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kukabiliana na uhalifu lakini ametaka juhudi hizo ziongezwe hususani kukabiliana na matukio ya uhalifu na uvunjaji wa amani,Msikilize hapa chini akiongea na Makamanda hao pamoja na IGP Sirro