Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Moses Sikawa amepata ajali ya pikipiki na kujeruhiwa vibaya wakati akielekea nyumbani kwake. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajli hiyo wamesema kijana huyo alianguka kutokana na kupita njia isiyoruhusiwa (wrong site) huku akiwa mwendo kasi.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku eneo la KIA wilayani Hai,mkoani Kilimanjaro ikihusisha pikipiki yenye namba za usajili T.522 BUB aina ya TOYO.Majeruhi huyo alionekana akitokea Moshi kuelekea Arusha huku akikimbizana na gari ambalo halikutambulika kwa haraka na alipofika eneo la KIA stendi ndipo akajaribu kulihepa gari kwa kupitia njia isiyoruhusiwa (njia ya kutoka Arusha kwenda Moshi) na haikumchukua muda akaanguka na kuumia sana.
Majeruhi aliwahishwa hospitali ya wilaya ya Hai kwa ajili ya msaada na matibabu zaidi.
MOSHI:MTU MMOJA AJERUHIWA VIBAYA KWA KUANGUKA NA PIKIPIKI
Reviewed by Unknown
on
12:05 PM
Rating: 5