BOFYA HAPA ILI KUJUA MADARAJA YA LESENI ZA UDEREVA
A - Pikipiki zenye ukubwa wa zaidi ya 125CC au uzito wa 230Kg ikiwa na kigari pembeni au isiyokuwa na kigari.
A1 - Pikipiki zenye ukubwa chini ya 125CC au uzito 230Kg na isiyokuwa na kigari pembeni.
A2 - Kuendesha pikipiki za magurudumu matatu au manne.
A3 - Mitambo ya kukatia majani au pikipiki zisizozidi 50CC.
B - Magari aina zote (Binafsi) *ISIPOKUWA* magari ya biashara, magari makubwa ya mizigo na pikipiki.
C - Magari ya kubeba abiria kuanzia 30 na kuendelea.
C1 - Magari ya kubeba abiria 15 hadi 29.
C2 - Magari ya kubeba abiria 4 hadi 14.
C3 - Magari ya kati ya abiria 4 hadi 14.
D - Magari aina zote *ISIPOKUWA* magari ya abiria, magari makubwa ya mizigo na pikipiki.
E - Magari aina zote *ISIPOKUWA* magari ya abiria na pikipiki.
F - Mitambo kama graders,folklift n.k
G - Mitambo ya mashambani na migodini kama tractors n.k
H - Leseni ya kujifunzia kuendesha gari.
NB: Unapokuwa na daraja D huna haja ya kuwa na daraja B kwa kuwa daraja D hujumuisha magari yaliyo katika daraja B ila ukiwa na daraja B huwezi endesha daraja D. Pia ukiwa na daraja A si kigezo cha kuendesha madaraja yote ya A,utaendesha madaraja yote ya A isipokuwa A2 ambayo ni pikipiki za magurudumu matatu/manne
Umri na madaraja ya leseni*
(i) Daraja A, A1,A2, B, D, F na G ni miaka 18 na kuendelea
(ii) Daraja A3 miaka 16 na kuendelea
(iii) Daraja C1,C2,C3, E ni miaka 21 na kuendelea.
Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za Sumatra za mwaka 2007 kif 17 (2) (b) dereva anayetakiwa kuendesha basi la abiria (PSV) anatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 60.
Daraja C kuanzia miaka 24 lakini kwa kanuni za Sumatra anatakiwa awe na miaka 30 hadi 60.
Weka maoni/ushauri wako hapa nasi tutaufanyia kazi.