MKUU
wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro kwa mara ya kwanza amefanya
mazungumzo maalum na wanahabari jijini Dar es Salaam na kutangaza dau
nono la Sh10 milioni kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti,
Rufiji na Mkuranga.
“Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo.
Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi.
“Huu ni wakati wa kutii utawala wa sheria bila shuruti na nimeshaongea na makamanda wa polisi nchi nzima,” amesema. Bofya hapa chini kumtazama
VIDEO:IGP SIMON SIRRO KAONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KWA MARA YA KWANZA NA KUTANGAZA DAU LA MILIONI 10
Reviewed by Unknown
on
9:14 PM
Rating: 5