Timu ya Azania imeondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ajili
ya kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield
yatakayofanyika kwenye uwanja wa klabu ya Liverpool wa Anfield. Timu hiyo imeondoka na msafara wa watu 10 ambapo kati yao wachezaji
ni saba ambao ni Shabaka Hamisi, Rajabu Ally, Akhamedy Afifu, Abdala
Khalidi, Thomas Bishanga, Alidi Said na Brayan Dobadi. Wachezaji
wa Timu ya Azania wakibadilishana mawazo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kukwea
pipa kuelekea nchini Uingereza.Azania itashiriki mashindano hayo ikiwa ni mabingwa wa kombe la
Standard Chartered Safari kwenda Anfield kwa Afrika Mashariki na Kati na
ikiwa kwenye mashindano hayo itakutana na timu zingine kutoka Botswana,
Nigeria, Hong Kong, Korea, Singapore, India pamoja na Uingereza. Timu hiyo itafika Uingereza Mei, 19 wakiwa huko watakutana na timu
zingine, Mei, 20 watatembelea uwanja wa Anfield, Mei, 21 watashuhudia
mchezo wa Liverpool na Middlesbrough na baada ya hapo wataingia uwanjani
kwa ajili ya mashindano na watarejea nchini Mei, 22. Mariam
Sezinga (kushoto) wa Benki ya Standard Chartered Tanzania akiongoza
msarafa huo wa timu ya Azania kuelekea nchini Uingereza.Kikosi
cha Timu ya Azania katika picha ya pamoja na kiongozi wa msafara huo
Mariam Sezinga (wa kwanza kushoto) wa Benki ya Standard Chartered nchini
kabla ya kuingia lango kuu la kusafiria katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Timu ya Azania wakiingia ku-‘check in’ tayari kukwea pipa kuelekea nchini Uingereza.Mariam
Sezinga (kulia) wa Benki ya Standard Chartered Tanzania akihakikisha
hati zote zimekamilika tayari kwa ku-‘check in’ katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Timu ya Azania wakiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Dubai usiku wa kuamkia leosafarini kuelekea nchini Uingereza.
TIMU YA AZANIA YAONDOKA NCHINI KUELEKEA UINGEREZA
Reviewed by Unknown
on
11:37 PM
Rating: 5