Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam imesema tayari
imewasiliana na shirikisho la kimataifa la vyama vya mpira wa miguu
duniani FIFA kuhusu malalamiko ya kutokutendewa haki katika mfumo mzima
wa uendeshaji wa mpira wa miguu hapa nchini.
Makamu wa rais wa Simba, Geofrey Nyange maarufu kama Kaburu amesema
baada ya kupokea barua ya kunyang'anywa alama tatu kwa sasa wanajiandaa
rasmi kwenda FIFA kwaajili ya kuwasilisha malalamiko yao na wanaamini
kupitia FIFA haki yao itapatikana.
Aidha Kaburu amewataka wanachama wa Simba kuwa watulivu kwani timu
hiyo ina fedha za kutosha kugharamia kesi hiyo pindi itakapofikishwa
rasmi FIFA.