SERIKALI YAAHIDI NEEMA TAASISI ZA KIDINI.
Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi,
Mhashamu Isack Amani akimuombea rais Dkt. John Magufuliibada wakati wa
ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu Kristo Mfalme Jimbo
Katoliki Moshi
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akishiriki ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu Kristo Mfalme Jimbo Katoliki Moshi pamoja na Kanisa la KKKT Usharika wa Moshi Mjini.
Katika Kanisa la KKKT Usharika wa Moshi Mjini , Askofu Mkuu wa KKKT Dkt. Fredrick Shoo amemuomba Rais John Magufuli kuwapunguzia kodi katika vifaa wanavyoagiza kwa ajili ya kutolea huduma kwenye Taasisi za dini.
Akiwa katika Kanisa la Kiaskofu la Kristo Mfalme Jimbo Katoliki Moshi, Rais Magufuli amesisitiza suala la amani na upendo.
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi, Mhashamu Isack Amani ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Rais Magufuli ametoa mifuko mia mbili ya saruji na shilingi milioni mbili kwa kwaya katika makanisa hayo.


