Msanii Rama Madee amesema
yeye ni kati ya watu ambao wanamkubali Rais Magufuli kutokana na
uthubutu wa kiongozi huyo katika kufanya mambo yake ambayo kama kweli
atayasimamia na kuyafanyia kazi kiuhalisia basi yatasaidia nchi kupiga
hatua zaidi.
Rama
Dee amesema hayo katika kipindi cha KIKAANGONI ambacho kinarushwa
kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa
nane mpaka saa kumi jioni
"Mimi kiukweli namkubali
sana Rais Magufuli kwani hapo alipoanzia ni pazuri, hivyo sina tatizo
kabisa na uongozi wa awamu ya tano, kuna kauli ambazo Mh. Rais Magufuli
huwa anazitoa unaona kabisa ni mtu ambaye anathubutu kutenda, mfano
hapindishi anasema kabisa ili tuweze kufanikiwa lazima tufanye kazi,
hivyo sasa ni jukumu la serikali kuona inatengeneza namna nzuri hao
vijana ili waweze kupata hizo ajira, watu wakapata huduma nzuri
kulingana na kodi wanazolipa" alisema Rama Dee
Rama alisisitiza kuwa kama kauli hizo za Rais Magufuli atazifanyia
kazi na serikali ikatengeneza mifumo mizuri katika kila kitu basi
anaamini nchi itasonga mbele.
"Kwa kuwa Rais ameonyesha huo uthubutu sasa ni jukumu la serikali kutenda kweli, hayo mambo ili tuweze kusonga mbele zaidi"alisisitiza Rama Dee
RAMA DEE AFUNGUKA JINSI ANAVYOMKUBALI RAIS MAGUFULI.
Reviewed by Unknown
on
7:11 AM
Rating: 5