RAIS MAGUFULI ATIMIZA NDOTO YA ZITTO KABWE...CHEKI ALICHOKIAMUA

Siku moja baada ya Rais Magufuli kuzuru kituo cha shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC), Nakuagiza kupitiwa upya mkataba wa uliongiwa baina ya
shirika hilo na kampuni ya kichina ya Startimes, Basi Mbunge wa Kigoma
mjini Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika hivi...
"Nasikia Rais kaagiza kuhusu Mkataba wa StarTimes na TBC. Mwaka 2011 tulipata kuazimia Hivi;
"7.2.10 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mkataba baina ya Shirika la
Utangazaji Tanzania ( TBC) na Star Times International Communication una
mapungufu kadhaa ya kisheria na ambayo yamebainishwa na Mkaguzi wa
Hesabu wa TBC baada ya kuchambua Mkataba na Taarifa ya Hoja za
Ukaguzi,na kwa kuwa mapungufu hayo yanaweza kuwa na athari katika
utendaji wa TBC kwa siku zijazo , kwa hiyo basi Kamati inapendekeza
kuwa, Serikali iupitie upya Mkataba huo ili kuainisha maeneo ya
maboresho, aidha Serikali ifanye utaratibu wa kuangalia namna nzuri ya
kutoa fedha kwa uendeshaji wa TBC ili kiwe chombo cha utangazaji wa Umma
chenye kujiendesha kwa uhuru na kwa maslahi ya Umma."


