Maafisa wa forodha
nchini Kuwait wamemkamata njiwa aliyekuwa amebeba madawa ya kulevya
katika mkoba mdogo mgongoni, gazeti la Kuwait, la al-Rai limeripoti.
Jumla ya tembe 178 ziliipatikana katika mfukop huo uliokuwa umepachikwa mgongoni mwake, gazezi hilo lilisema.
Ndege huyo alinaswa karibu na jumba la forodha jijini Abdali, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Iraq.
Mwanahabari
wa Al-Rai alisema kuwa madawa hayo ya kulevya yalikuwa aina ya
ketamine, nusukaputi ambayo pia hutumiwa kama dawa haramu katika
sherehe.
Abdullah Fahmi aliiambia BBC kwamba maafisa wa forodha
walijua mbeleni kuwa njiwa walitumiwa kusafirisha madawa ya kulevya,
lakini hii ilikuwa mara ya kwanza kunasa njiwa katika harakati hizo.
Maafisa wa utekelezaji wa sheria katika nchi
nyingine, wamewahi kuripoti visa vya njiwa waliodaiwa kutumiwa
kusafirisha madawa ya kulevya ya bei ghali japo kwa viwango vidogo.
Mwaka
wa 2015, askari wa magereza jijini Costa Rica walimnasa njiwa aliyekuwa
amebeba madawa ya kulevya aina ya kokeni na bangi kwa kipochi.
Na
mwaka wa 2011, polisi wa Colombia walimpata njiwa ambaye alishindwa
kuruka juu ya ukuta mrefu wa jela kwa sababu ya uzito wa mzigo wa
madawa ya kulevya ya kokeni na bangi aliyopachikwa.
Njiwa wametumika kupeperusha ujumbe tangu enzi za Waroma, wakitumia uwezo wao wa kurudi nyumbani walikotoka.
NJIWA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI KUWAIT
Reviewed by Unknown
on
7:29 AM
Rating: 5