MAZISHI YA IVAN SEMWANGA "THE DON" LEO TAREHE 30/05/2017
Mzazi mwenzie na Zari Hassan, IVAN SEMWANGA, anazikwa leo mjini Kampala baada ya misa ya kumwombea kufanyika siku ya jana Jumatatu.
Katika misa ya mazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Namirembe mjini Kampala, Zari alionyesha ujasiri alipoongea mbele ya umati na kueleza kuwa atawalea wanae hadi Mungu atakapomkutanisha tena na mzazi mwenzie huyo.
Zari baada ya kuachana na Ivan amezaa watoto wawili na mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania.



