LOWASSA ALALAMIKA HATUA YA SERIKALI KUZUIA KONGAMANO LA DEMOKRASIA...FUATILIA ZAIDI HAPA.

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema amesikitishwa na hatua ya
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ya kuzuia kongamano la demokrasia
lililopangwa kufanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Anatouglou.
Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alitoa kauli hiyo leo
(Jumamosi) wakati akizungumza na wanahabari ofisi kwake Mikocheni.
Amesema amelaani kitendo hicho na kusema kongamano hilo halikuwa na nia
mbaya bali lilikuwa limelenga kujadilia mambo mbalimbali kwa
mustakabali wa Taifa.
"Nimesikitishwa na kitendo hiki na nimeshangaa kwa jambo hili halikemewi.Nchi hii ni moja na kila mtu ana haki.
"Walituzuia mikutano ya hadhara tumetii, tumeamua kufanya mikutano ya
ndani wanatufuata fuata,"amesema Lowassa ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa
Monduli kwa nyakati tofauti.
Katika mkutano huo Lowassa aliambatana na mwenyekiti wa kamati ya
Maandalizi ya kongamano hilo Dk Makongoro Mahanga ambaye alishangazwa na
hatua hiyo ya Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam.


