KAMA ULIKUWA HUJUI...MSIKIE GABO ALICHOKISEMA KUHUSU YEYE NA WEMA SEPETU
Gabo Zigamba amefunguka kwa kudai kuwa picha za kimahaba zilizozagaa
mitandaoni akiwa na Wema Sepetu ni maandalizi ya kazi yao mpya na siyo
mambo mengine
Muigizaji huyo ambaye anafanya vizuri kwa sasa katika tasnia ya filamu,
amedai filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Heaven Sent’ ni full mahaba
ndio maana picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinawaonyesha
wakiwa katika hali isiyo ya kawida.
“Movie tunayoifanya na Wema iko very romantic ndio maana hata picha
zenyewe lazima ziwe hivo sasa watanzania naona wao washarasimisha kwamba
kuna kitu kinaendelea kumbe hakuna pale tupo kazini na niwaahidi
mashabiki zangu naandaa kitu kikali sana mara mbili za jinsi
wanavyonifahamu,” alisema Gabo.
Pamoja na hayo Gabo amewataka mashabiki wa filamu waendelee kuwapatia
changamoto za kejeli ikiwa ni pamoja na kusisitiza kazi nzuri ili
wasanii wasibweteke isipokuwa kutoa lugha za matusi.