HOUSE GIRL DAR AJIUA KWA KUJICHOMA KISU
Katika
hali isiyo ya kawaida dada wa kazi aliyetambulika kwa jina la Christina
Mabuga (37), amekutwa ameuawa ndani ya chumba chake, huko Moshi Baa,
Gongo la Mboto, Dar es Salaam kwa kujichoma kisu kifuani.
Jeshi
la Polisi katika mkoa wa kipolisi Ilala limethibitisha kutokea kwa
tukio hilo, lililofanyika katika nyumba ya mwajiri wa dada huyo wa kazi,
ambapo mpaka sasa haijafamika chanzo cha dada huyo kujiua.
Mwajiri
wa binti huyo, Anna Kasanda alisema alipokea taarifa saa 9:00 alasiri
kwamba kuna tatizo nyumbani kwake, na ndipo alipoamua kurudi nyumbani na
kukuta mfanyakazi huyo amejiua.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.