Utajiri wa Ivanka Trump na mumewe Jared Kushner ni hatari.
Wawili hao wana mali zenye thamani ya dola milioni 740. Hilo limewekwa
wazi na Ikulu ya Marekani kama sheria inavyowataka viongozi wa nchi hiyo
kuweka wazi mali zao.
Ivanka aliteuliwa siku chache zilizopita kwenye cheo cha msaidizi wa
Rais kama mwajiriwa asiyelipwa mshahara huku mumewe akiteuliwa mapema
mwaka huu kuwa mshauri mkuu wa rais. Naye mshauri mkuu wa Trump kuhusu
uchumi, Gary Cohn ametajwa kuwa na utajiri wa takribani dola milioni
250.
Inadaiwa kuwa watu waliopo kwenye baraza la mawaziri la Trump wana jumla ya mali zenye thamani ya dola bilioni 12.
UTAJIRI WA IVANKA TRUMP NA MUWEWE NI HATARI...SOMA ZAIDI HAPA
Reviewed by Unknown
on
4:32 PM
Rating: 5