TAARIFA KUTOKA BUKOBA:ZAIDI YA WATU 70 WAOKOLEWA LEO KUTOKANA NA MAFURIKO YALIYOTOKANA NA MVUA KUBWA.
Zaidi
ya watu 70 wameokolewa na Serikali baada ya kukumbwa na mafuriko
yaliyotokana na mvua iliyoanza kunyesha kuanzia saa 9 usiku.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo
wakati alipo hojiwa na waandishi wa habari katika Kata ya Bakoba mtaa wa
nyakanyasi.
Kinawilo alisema kuwa nyumba zote zilizoko kandokando ya mto kanoni zote
zimeathiriwa na maji kiasi kwamba imetumika mitumbwi ya uvuvi kuvusha
watu.
“Niseme tu mpaka sasa hakuna kifo chochote kile Zaidi ya vitu kuharibika kwa kulowa maji”alisema Kinawilo
Aidha mkuu wawilaya alisema kuwa kuwa wananchi wachukue tahadhari pindi
mvua zinapo nyesha tu watoke nje ya nyumba kwa usalama Zaidi.
Naye Josefati Bonge mkazi wa Omukigusha alisema kuwa katika nyumba yake
hakuna kilichobakia kikiwa kizima kwani ametoka yeye kama alivyo na anamshukuru Mungu familia yake haikuwepo.
“Kiukweli kuna kila sababu ya kuhama maeneo kama haya maana nihatari kwa
binadamu mfano’ waliokuwa wamelala fofofo wanahali gani hivyo kunatakiwa
kuchua hatua mapema ili kuhamia sehemu stahiki”alisema Bonge
Anitha Mziba mkazi wa Nyakanyasi alisema kuwa yeye katika familia yake
hakuna alieumia Zaidi ya vitu vyote vya ndani hakuna kilichotoka.
“Yani
nimewabeba watoto wangu begani mmoja baada ya mwingine wakati huo mimi
maji yakiwa yamenifikia kwenye shingo kwakweli nihatari”alisema Mziba
Wakaazi wa hapa Tangu usiku saa 9 waliondoka!
Mkazi
wa Omukigusha akisaidiwa kuvutwa juu baada ya kuanguka shimoni asubuhi
leo kwenye mufda wa saa nne.
Prince Motel
Crane Lodge and Tours
Hii ni nyumba ya Wageni...lakini inasemekana Usiku hawakupata usingizi kabisa!
Hivi ndivyo ilivyokuwa Asubuhi ya leo
Eneo la Ziwa Victoria...Ufukweni
Ufukweni Ziwa Victora
Patashika wakazi wakiokoa Nyasi kwa ajili ya Mifugo yao
Mkazi wa Nyakanyasi akivuka huku akiwa hana matumaini Aendako
Katikati ya Makazi ya watu Eneo la Nyakanyasi Mitumbwi imefanya kazi
Okoa okoa ikiendelea eneo la Nyakanyasi Mjini Bukoba leo hii