PANGA LA TCRA LAZIUMIZA VODACOM,HALOTEL,TTCL NA NYINGINEZO....ZATOZWA FAINI YA MIL.65.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya milioni 65
kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi baadhi ya
vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya 9,10 na 11
ya kanuni za ubora wa huduma za 2011
Akiongea jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alizitaja
kampuni hizo kuwa Benson Informatics Limited Smart, Airtel Tanzania,
Vodacom Tanzania, Zanzibar Telecom Limited "Zantel", Mic Tanzania Limited,
Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania Telecommunications
Company Limited, TTCL huku akizitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa
huduma bora.
"TCRA
inawakumbusha watoa huduma wote wa mawasiliano nchini kuhakikisha
mnatoa huduma zinazokidhi ubora wa sauti na upakuaji wa hali ya juu
(Kudownload) pamoja na kufuata sheria za huduma ya mawasiliano ya mwaka
2011". Alisema Kilaba
Aidha Mhandisi huyo alisema wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma kama ilivyo agizwa.