Nape Nnauye Amlilia Roma Mkatoliki...Tazama Alichokiandika Mtandaoni.

Nape
emetoa kilio chake kupitia ukurasa wake wa Twitter, akitumia maneno
matatu pekee yanayosomeka kwa hisia za ndani kuwa ni mtu anayemlilia
mpendwa wake.
“Roma! Oooooh No!” ametweet Nape.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na uongozi wa Tongwe Records,
watekaji walifika katika studio hizo na kuwahoji waliokuwepo, kisha
kuondoka nao wote pamoja na baadhi ya vifaa vinavyotumika kurekodia
muziki, kwenda kusikojulikana.
Mke
wa Roma, Nancy ameeleza kuwa alifika katika vituo kadhaa vya polisi
jijini Dar es Salaam kuulizia taarifa za mumewe, lakini alielezwa kuwa
taarifa za Roma hazikuwepo.
Akizungumza
kwa uchungu kwenye vyombo mbalimbali vya habari, Nancy aliwaomba
Watanzania kwa ujumla pamoja na vyombo vya usalama kusaidia kufahamu
alipo mumewe.
Leo
mchana, wasanii wamekutana katika studio za Tongwe Records kwa lengo la
kuzungumzia suala hilo zito ambalo limevunja mioyo ya wadau wa muziki,
familia na ndugu wa Roma na wenzake.


