Baada ya msanii wa hip hop Roma
Mkatolikia kukamatwa akiwa na wenzake katika studio za Tongwe zilizopo
Masaki jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini atoa
agizo kwa polisi kufuatilia jambo hilo.
Roma na wenzake walikamatwa April 5 usiku
ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa
alikamatwa na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa
kusikojulikana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu
Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake
wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na
Moni.
Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la kutekwa kwa wasanii hao.
“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa
Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na
kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza
Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao
na kutoa taarifa kwa umma”.
Mwigulu Nchemba Atoa Neno Kutekwa Kwa Roma Mkatoliki.
Reviewed by Unknown
on
12:07 PM
Rating: 5