Marianne Mdee aka Mimi Mars amepitia vikwazo vingi katika
kutafuta tobo kama ambavyo wasanii wengine wamepitia licha ya yeye kuwa
mdogo wake na Vanessa Mdee.
Akiongea kwenye kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, Mimi alisema
Lulu na Wema Sepetu waliwahi kumtosa kumpa shavu kwenye movie.
“Nilishawahi kumuomba Lulu, Elizabeth Michael nakumbuka tuliwahi
kuongea naye hata akina Wema kuomba kuingiza kwenye bongo movie lakini,
Vanessa ndio alikuwa ananisaidia kuongea nao lakini kama walinipiga
chini fulani hivi but it’s okay,” alisema.
Hata hivyo Mimi hana kinyongo nao kwakuwa kipindi hicho alikuwa
hajulikani na anaona ni kitu cha kawaida. Anasema wawili hao kwa sasa ni
marafiki zake.
Mimi Mars Adai Lulu na Wema Waliwahi Kukataa Kumpa Shavu kwenye Movie
Reviewed by Unknown
on
6:43 AM
Rating: 5