Waigizaji wa Movie wamepata fursa ya
kuanza kuuza filamu zao nchini China ambao sasa zitakuwa zikitafsiriwa
kwa lugha ya nchi hiyo.
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Michezo,
Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye aliwaombea wasanii hao kwa serikali ya
China ambapo maombi hayo yalipokewa kwa mikono miwili.
Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini,
Simon Mwakifwamba alisema wamepanga kuanza kutengeneza filamu zenye
viwango vya juu ili kuweza kukimbizana na soko hilo lenye idadi ya watu
zaidi ya bilioni moja.
China imezindua wiki ya filamu zake hapa
nchini ambapo kazi hiyo inasimamiwa na kampuni ya ving’amuzi ya Star
Times ambapo uzinduzi huo ulifanywa na Nnauye .
MATUNDA YA NAPE NNAUYE KWA BONGO MOVIE HAYA HAPA....WAPATA SHAVU NONO CHINA.
Reviewed by Unknown
on
6:45 PM
Rating: 5