Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale
amempa makavu mkurugenzi wa Global Publisher, Eric Shigongo baada ya
kuandika habari kuhusu Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Babu Tale amefunguka mazito kuhusu mwanzo
wa tofauti zao na mkurugenzi huyo huku akidai kuwa biashara ndiyo
imechangia tofauti zao.
Kupitia akanti yake ya Instagram Babu ameandika maneno yafuatayo.
Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara
yangu kwenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na
kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya.
Baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na
kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi
kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako.
Siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku
vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa
unacholazimisha kukipata.
Ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa
magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya
kwa wasanii wangu, wasanii wengine na watu mbalimbali.
Tafadhali heshimu biashara yangu kama
inavyokuheshimu… Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya
Diamond… ila sie tume kaa kimya… na kujifanya unazuga eti unatushauri.
Kweli mtu unasema unampenda unamshauria
instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?….. Mbona sie
hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza
bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini?
…na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka
kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost.
Ila baada ya kuona watu wameipokea kwa
ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe,
eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa….tukaona tukae tu kimya, na
hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia
kubwa.
hivi kweli hata kama kuweka wasanii
karibu na amshabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao
kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii
wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika
wewe….mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa.
Yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama
kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo
za uongo na kweli ili kum’bomoa msanii kupitia magazeti
yako…..tafadhali heshimu heshima yetu kwako👍……
“Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao…..😓
KUMBE UGOMVI WA BABU TALE NA SHIGONGO CHANZO KIKUU KIPO....MSIKILIZE TALE HAPA ALIVYOFUNGUKA YOTE.
Reviewed by Unknown
on
6:56 PM
Rating: 5