Marais wa China na Marekani Wafanya Mazungumzo.
Katika mazungumzo yao, marais hao wamesifu maendeleo ya uhusiano kati ya nchi zao na wamekubaliana kuusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo upate mafanikio makubwa zaidi na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili na watu wa nchi zote duniani.
Rais Xi amesema ushirikiano ni chaguo pekee sahihi la China na Marekani, nchi ambazo zinaweza kuwa wenzi wazuri wa ushirikiano, na kwamba pande hizo mbili zinapaswa kupanga mawasiliano kati ya viongozi wa nchi hizo. Rais Xi amemkaribisha rais Trump kufanya ziara rasmi nchini China ndani ya mwaka huu.
Rais Trump amesema Marekani na China zinabeba majukumu makubwa kwa kuwa nchi kubwa kiuchumi duniani, hivyo pande hizo mbili zinapaswa kufanya mawasiliano na uratibu katika masuala muhimu ili kupata mafanikio makubwa zaidi.


