Timu ya soka ya AC Milan ya Italia imeuziwa kampuni ya China na
kufikia kikomo umiliki wake na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo
na tajiri Silvio Berlusconi.
Kampuni ya China Rossoneri Sport Investment Lux, imekamilisha mkataba
wa kuinunua timu hiyo kwa kima cha dola milioni 628, huku ikiwa na
matumaini ya "kuongeza faida mara dufu".
Klabu hiyo ya Serie A imekuwa chini ya umiliki wa bilionea Silvio Berlusconi, tangu mwaka 1986.
Katika kipindi hicho chote, AC Milan ilifaulu kunyakua mataji
manane katika ligi kuu na kutwaa kombe la vilabu bingwa barani Ulaya
mara tano.
Aidha, Milan haijawahi kushinda mechi za Seria A tangu mwaka 2011
na imemaliza katika nafasi ya 7, 10 na 8 katika misimu mitatu
iliyopita.
Kwa sasa inashikilia nafasi ya 6 katika ligi kuu, alama 20 nyuma ya vinara Juventus.
AC Milan Yanunuliwa na Kampuni ya China.
Reviewed by Unknown
on
9:27 AM
Rating: 5