TANZIA: MBUNGE DKT. ELLY MARKO MACHA AFARIKI DUNIA
Mbunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Viti Maalum
(CHADEMA) akiwakilisha walemavu Dkt. Elly Macha amefariki dunia baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, Dkt Macha amefariki
katika hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa
akipatiwa matibabu.
Taarifa
hiyo imesema kuwa mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kuja nchini
ikiwa ni pamoja na taratibu za mazishi inaendelea kufanywa na Ofisi ya
Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu.



