Serikali Yaagiza Nay wa Mitego Aachiwe Huru na Wimbo Wake Uendelee Kuchezwa Redioni.

Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe,
ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego ambaye
alikuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.
Waziri
Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo wa
‘WAPO’ na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Akiongea
na Wandishi wa Habari Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli
amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO na kumshauri Msanii huyo kama
inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile wakwepa Kodi, wauza
Unga, wanaotumia dawa za kulevya pamoja na watu wengine wasio na maadili
mema katika jamii.


