Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan
Kikwete amempngeza Mama yake baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa
Mbunge wa viti maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ridhiwan Kikwete amesema kuwa mama Salma
Kikwete ni mwanamke wa shoka kwani amewezesha wasichana wengi nchini
Tanzania kupata elimu na amekuwa mtetezi wa haki za wanawake hivyo
anaamini kupata nafasi ya kuwa Mbunge itakwenda kuwezesha mapambano kuwa
sheria rasmi.
Kupitia akaunti yake Instagram Ridhwani
ameandika “Umekuwa mtetezi wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia,
umewezesha wasichana kupata elimu. Wewe ni mwanamke wa Shoka. Hongera
sana kwa uteuzi. Imani sasa umepata sehemu ya kuwezesha mapambano kuwa
sheria. Mungu akutangulie Mama yangu , Mheshimiwa Mbunge. Hongera tena”.
Ridhwani ampongeza Mama Salma Kikwete kuteuliwa kuwa mbunge
Reviewed by Mipiko
on
3:51 PM
Rating: 5