Jeshi la Polisi kwa mara nyingine Jumatano hii ilizingira
nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa
kile lilichodai kuwa lilifika kufanya uangalizi.
Akizungumza kwa simu na gazeti la Mtanzania jana, Askofu Gwajima alikiri polisi hao kumfuata nyumbani kwake na hivyo kulazimika kumtafuta wakili wake mara moja.
“Ni kweli walikuja wakiwa na gari la polisi, lakini walipofika nami
nilimpigia mwanasheria wangu ambaye aliniambia tuwaulize wametumwa na
nani na kama wana ‘search warrant’ (kibali cha kufanya upekuzi) au
‘arrest warrant’ (kibali cha kukamata),” alisema.
Aidha Askofu Gwajima alisema walipowauliza, walimtaja Afande Kingai
kama ndiye mtu aliyewatuma, lakini hawakuwa na kibali chochote. Kwa
mujibu wa Askofu Gwajima, mwanasheria wake alifanya mawasiliano ya simu
na Afande Kingai ambaye amepewa jukumu la kuwafuatilia wale wote
waliotuhumiwa katika sakata la dawa za kulevya na kumuuliza sababu za
kumfuata nyumbani.
“Afande Kingai amemweleza mwanasheria wangu kuwa walikuwa wamekuja
kwa ajili ya ‘observation’ (uangalizi) tu, kwahiyo mwanasheria wangu
akasema kama ni ‘observation’ tu tusiwaruhusu kuingia ndani kwa sababu
sheria ya hivyo hakuna, na sisi tumewazuia hawakuingia ndani,” alisema
Askofu Gwajima.
Askofu huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameiweka habari hiyo.
Polisi Wazingira nyumba ya Askofu Gwajima usiku
Reviewed by Mipiko
on
3:59 PM
Rating: 5