Rais wa China Apongeza Ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Bo'ao.
Rais Xi amesema miaka 16 tangu Baraza la Asia la Bo'ao lianzishwe, baraza hilo limetoa mchango muhimu katika kufikia maoni ya pamoja barani Asia, kuhimiza ushirikiano, na kuongeza ushawishi wa Asia.
Rais XI amesisitiza kuwa kaulimbiu ya mkutano huo ya "Kukabiliana na utandawazi duniani na mustakabali wa biashara huria", inaonesha ufuatiliaji wa jumuiya ya kimataifa haswa nchi za Asia, juu ya mafungamano ya kiuchumi duniani.
Pia rais Xi ameeleza matumaini yake kuwa, washiriki watachangia busara zao kwa ajili ya kutatua matatizo makubwa yanayoukabili uchumi wa kikanda na duniani, kuhimiza kwa pamoja mchakato wa utandawazi ulio endelevu, wenye uhai na mapatano zaidi.


