Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana amekutana na waziri mkuu wa
Australia Bw. Malcolm Turnbull, ikiwa ni mara ya tano kwa mawaziri hao
kukutana.
Katika mazungumzo yao, Bw. Li Keqiang amesisitiza kuwa pande hizo
mbili zinapaswa kushughulikia vizuri kazi ya kuthibitisha makubaliano
kuhusu biashara huria, kufanya majadiliano ya kina kuhusu sekta za
biashara ya utoaji wa huduma na uwekezaji, na kupanua biashara huria
katika sekta nyingi zaidi, ili kuhimiza mchakato wa utandawazi wa uchumi
duniani na uwekezaji wa biashara huria, na kujenga uchumi wa dunia ulio
wazi kwa nje.
Bw. Turnbull amepongeza juhudi za China katika kuhimiza
utandawazi wa uchumi duniani, na kuhimiza ufunguaji zaidi wa soko kwa
nje. Pia ameeleza kuwa anatumaini kushirikiana na China kukuza
mawasiliano, kupanua ushirikiano ili kuhimiza nchi hizo mbili hata nchi
zote duniani kupata amani na ustawi kwa pamoja.
Mawaziri Wakuu wa China na Australia Wakutana.
Reviewed by Unknown
on
8:26 AM
Rating: 5