Breaking News

Nape:Heshima aliyonipa Mheshimiwa Rais ni kubwa mno.


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnaye amemshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kumuamini na kumpa thamani kubwa kusimamia wizara hiyo kwa miezi 15 huku akisema heshima aliyompa ni kubwa mno.

Mheshimiwa Nape ambaye ni mbunge wa Mtama ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika makao makuu ya wizara hiyo yaliyopo mkoani Dodoma.
“Heshima aliyonipa Mheshimiwa Rais ni kubwa mno nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini. Tofauti na maneno yanayosemwa mtandaoni mimi nitakuwa mtiifu kwa Rais, serikali na chama changu.”