Mwigulu Nchemba Aagiza Aliyemtishia Bastola Nape Nnauye Akamatwe.
Mheshimiwa Mwigulu ameahidi kumsaka askari huyo ili sheria ifuate mkondo wake.
“Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu,” ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram.
“Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini,” ameongeza.
“Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.”
Kabla ya kuanza kuzungumza na waandishi wa habari, Nape alizuiliwa na askari kadhaa walionekana kwenye video wakimlamzimisha arudi ndani ya gari lake kabla ya mmoja kuchomoa bastola.
“Kwanini mnatoa bunduki hadharani, mimi jambazi?” alihoji Nape.


