Kiongozi
mwanaharakati aliyeshiriki sana kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa
rangi nchini Afrika Kusini Ahmed Kathrada amefariki dunia akiwa na umri
wa miaka 87, wakfu wake umetangaza.
Bw Kathrada alifariki dunia
akiwa katika hospitali moja mjini Johannesburg "baada ya kuugua kwa muda
mfupi, kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwenye ubongo wake".
Pamoja
na Nelson Mandela, Bw Kathrada alikuwa miongoni mwa wanaharakati wanane
wa African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka
1964.
Walipatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi.
Bw Kathrada alikaa jela miaka 26, 18 kati ya miaka hiyo akiwa katika gereza hatari la Robben Island.
Aliachiliwa huru mwaka 1989.
Rais Mandela baadaye alimshawishi kujiunga na serikali.
Ahmed Kathrada aliondoka bungeni 1999, lakini aliendelea kushiriki katika siasa nchini humo.
Alikosoa mwelekeo wa chama cha ANC hivi majuzi na kumtaka Rais Jacob Zuma kujiuzulu.
Mwanaharakati Kathrada wa Afrika Kusini afariki Dunia.
Reviewed by Unknown
on
9:26 AM
Rating: 5