Mfalme wa miduara nchini Tanzania
AT ambaye kwa sasa anatamba na ngoma mpya yenye mahadhi tofauti na
mduara inayokwenda kwa jina la ‘Sili feel’, amemtaka msanii Tundaman
kuanza kucheza ‘mauno’(dansi) ili aweze kupata ‘kiki’ mjini.
Hayo yameibuka baada ya Tundaman kulalamikia vyombo vya habari pamoja
na blog kuwapa ‘promo’ nyingi wasanii ambao hawana sifa stahiki huku
wenye vipaji kuachwa.
“Kitu cha kwanza inatokana na jambo ambalo lipo wazi, wa
muziki wa dansi wenzetu nyimbo zao hawapeleki katika ‘media’ ila
zinatafutwa, pia kaka yangu Tundaman wakati alipokuwa anazungumza
alisema kuna wasanii wabovu ndiyo wanapata promo lakini angejaribu
kuweka sawa, wanaopewa promo siyo wasanii wabovu, aseme madansa ndiyo
wanapata promo”– Alisema AT kupitia kipindi cha Enewz kutoka EATV
Msanii huyo aliendelea kumrushia vijembe Tundaman kwa kumwambia kama
naye anahitaji ‘promo’ abadili uraia awe mkongo ama atazame njia
nyingine ya kutokea nasio kupiga soga tu.
Vile vile amesema ni jambo baya kwa msanii kama yeye kuanza
kulalamika ‘promo’ wakati yeye mwenyewe yupo jikoni anapaswa kujipika,
huku akimtolea mfano wa mama ntilie anayepika chakula na kupakua chote
bila kuambulia hata ukoko.
“Madansa ndiyo wanapata ‘promo’ kwa hiyo kama anaweza
kubadili uraia nyimbo zake zikatafutwa sawa, ila kama atashindwa atafute
njia nyingine ya kutokea kwasababu hata yeye yupo jikoni, hata ukoko
atakosa ?, hii mambo inakuaje si hatari hii”. Alisisitiza AT
Kwa upande mwingine amesema kuna wasanii hawana vipaji ila wanabustiwa na mkwanja ili waonekane wazuri.
Msanii AT Amtaka Tundaman Kuhamia Kwenye ‘Mauno’ Ili Apate Kiki.
Reviewed by Mipiko
on
1:16 PM
Rating: 5