Kampuni ya McDonald’s ambayo ndiyo
wamiliki wa migahawa ya McDonald’s iliyosambaa maeneo mbalimbali duniani
imeomba msamaha kwa Rais wa Marekani, Donald Trump baada ya akaunti
yake ya Twitter kuweka maeneno ambayo yalikuwa yakimsema vibaya Trump.
Katika taarifa ambayo imetolewa na
kampuni hiyo ilieleza kuwa si wao ambao walifanya kitendo hicho bali ni
wahalifu wa mtandaoni (hackers) ambao walikuwa wameiba akaunti hiyo na
kuweka ujumbe huo ambao ni wazi haukuwa na maneno mazuri ya kufurahisha.
“Kwa uchunguzi ambao tumeufanya
tumebaini kuwa akaunti yetu ya Twitter ilikuwa imeibiwa. Tulichukua
hatua ili kuilinda, na tunaomba radhi kwa ujumbe ambao ulikuwa umewekwa
kwenye akaunti yetu,” alisema msemaji wa McDonald’s, Terri Hickey katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.
Ujumbe ambao ulikuwa umewekwa kwenye akaunti ya McDonald’s ulikuwa ukisema,”@realdonaldtrump kwa kweli Urais wako unatatiza sana, tunapenda arudi @BarackObama”
McDonald’s Yamwomba Radhi Rais Trump Kwa Kumwandika vibaya Mtandaoni.
Reviewed by Mipiko
on
1:23 PM
Rating: 5