Mwanamuziki chipukizi nchini, Harmorapa
amemuomba radhi Diamond baada ya akaunti yake ya Instagram kutumika
kumtukana mwanamuziki huyo.
Harmorapa kupitia akaunti yake ya
Instagram amepost kipande cha video kwenye mtandao huo akisema kitendo
hicho hakufanya yeye bali kuna watu walihack akaunti yake hiyo.
“Followers wangu, mashabiki wangu nasikitika kitu kimoja toka asubuhi leo (jana) nashindwa kuingia katika akaunti yangu,”.
“Kuna watu wamehack akaunti yangu na kupost vitu ambavyo sio vizuri
ni vyaajabu sana. Mimi binafsi siwezi kumtukana Diamond wala kumtukana
Alikiba pia na P Funk Majani ambaye nipo naye kwenye mizunguko yangu leo
kwa Mx Carter kwa kunisaidia kuirudisha akaunti yangu,” .
Mkali huyo ameamua kufanya hivyo baada
mashabiki kumshambulia kwa matusi kuhusu kumtukana Diamond kupitia
akaunti yake ya Instagram.
HARMORAPA AMPIGIA MAGOTI DIAMOND....NI BAADA YA AKAUNTI YAKE INSTA KUTUMIKA KUMTUSI MOND.
Reviewed by Mipiko
on
12:58 PM
Rating: 5